“Ushiriki wetu katika mkutano ulituwezesha kubadilishana uzoefu juu ya mada mbalimbali zilizojadiliwa, kujenga mitandao na kuanzisha ubia mpya na washiriki kadhaa. Vile vile, tuliweza kusajili washiriki wapya. Aidha, ilikuwa ni fursa ya kujifunza kwetu hasa juu ya uandaaji wa mikutano na juu ya teknolojia mpya zinazoibuka katika tasnia ya nishati safi na hii ni pamoja na uendelezaji wa nishati ya jotoardhi, hidrojeni safi, na juhudi za kupunguza hewa ukaa katika shughuli za uchimbaji madini, sekta ya uchakataji mafuta na gesi ghafi. Kwa ujumla, mkutano ulikuwa wa thamani kubwa sana kwa shirika letu.”
IMEANDALIWA CHINI YA UONGOZI WA MUHESHIMIWA DKT. DOTO MASHAKA BITEKO (MB), NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI, WIZARA YA NISHATI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KUONGOZA SEKTA YA NISHATI YA TANZANIA ILI IKIDHI MAHITAJI YA NISHATI KIKANDA NA KIMATAIFA
Karibu katika Mkutano wa Nishati Tanzania 2024
Kufuatia mafanikio ya Mkutano wa Nishati 2023, wandaaji wenza wa Mkutano wa Nishati ambao ni dmg Events na Ocean Business Partners Tanzania, wanayofuraha kukutangazia kuwa Mkutano wa 6 wa Madini Tanzania umeidhinishwa rasmi na utafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 11 – 12 Septemba 2024.
Tanzania inaendelea kukua kwa kasi kama nchi wezeshi ya kimkakati katika fursa mpya za kibiashara kwenye tasnia ya nishati Afrika Mashariki. Mwaka huu Mkutano utajikita katika kutoa mrejesho kuhusu maeneo muhimu ya sekta ya nishati Tanzania ikiwa ni pamoja na Mradi wa Kuchakata na Kusindika gesi Asilia (LNG), mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), Maendeleo ya gesi ya mkondo wa juu, pamaoja na mapendekezo mbalimbali ya miradi ya nishati jadidifu.
Ungana na wadau muhimu wa ndani, wa kikanda na wa kimataifa Septemba hii ili uwe sehemu ya simulizi ya mafanikio katika ukuaji wa nishati Tanzania.